Mbunge Namtumbo akabidhi mifuko ya smenti 40 na madawati 30.
Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Mkoani Ruvuma Vitta Rashid Kawawa amekabidhi mifuko ya simenti 40 na madawati 30 katika shule ya msingi Upendo .
Akikabidhi mifuko hiyo pamoja na madawati Kawawa alisema anatimiza ahadi yake aliyohaidi katika ziara yake ya tarehe 16.9.2023 alipotembelea Kijiji Cha Mputa na wananchi kumwomba msaada wa kuisaidia shule ya msingi upendo
Aidha Kawawa aliwashukuru wananchi wa Kijiji Cha Mputa Kwa ushirikiano wao wa kujenga shule ya msingi Upendo lakini akadai Ofisi ya Mbunge itahakikisha shule hiyo inapata fedha kama shule zingine .
Hata hivyo Kawawa alimwagiza Afisa elimu vifaa na takwimu aliyemwakilisha afisa elimu msingi katika makabidhiano hayo kuwa ofisi ya elimu msingi inatakiwa kutenga bajeti ya kujenga madarasa ,Nyumba za walimu na vyoo Kwa ajili ya shule hiyo
Pamoja na hayo Kawawa aliiagiza idara ya elimu kuwa ushiriki wao katika miradi ijayo ya boost Namtumbo wahakikishe shule ya msingi Upendo inapewa kipaumbele katika bajeti ya boost Ili kuondoa changamoto
Afisa elimu vifaa na takwimu Lulu Mapunda alimshukuru mbunge wa Jimbo la Namtumbo Vitta Rashid Kawawa Kwa kuisaidia shule hiyo madawati 30 na mifuko ya simenti mifuko 40 Ili kuisaidia shule hiyo kuboresha miundombinu yake.
Afisa elimu ,Elimu ya watu wazima Shaibu Majiwa pamoja na kumpongeza Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Vitta Rashid Kawawa Kwa upendo wake wa kusaidia huduma za jamii aliwaambia wananchi wa Kijiji Cha Mputa kuwa mbunge huyo ni mnyenyekevu,mpole na msikivu Kwa wananchi wake .
Majiwa alifafanua kuwa unyenyekevu wake akiwa bungeni humsaidia kuomba fedha za miradi na kuifanya Namtumbo kuwa na miradi mingi yenye fedha nyingi alisema Majiwa.
Shakimu Sudi Ngonyani akiongea Kwa niaba ya wazee wa Kijiji Cha Mputa alisema wazee wa Kijiji Cha Mputa wanamshukuru mbunge Kawawa Kwa jitihada yake ya kuisaidia shule hiyo pamoja na wananchi wa Jimbo la Namtumbo .
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Upendo Laika Hassan Ngonyani pamoja na kumshukuru Mh.Mbunge wa Namtumbo Vitta Kawawa Kwa msaada wake wa smenti mifuko 40 na madawati 30 aliendelea kumwomba mbunge huyo kuwa shule hiyo Bado inachangamoto ya Nyumba za walimu ,madarasa yenye sakafu ya vumbi huku akidai wananchi wamejenga Nyumba moja ya mwalimu Kwa nguvu zao na imeishia hatua ya linta ambapo Mbunge wa Jimbo Hilo akakubali Kutoa milioni tano(5,000,000) Kwa ajili ya kuweka ringbeam ya Nyumba ya mwalimu pamoja na kuezeka..
Shule ya msingi Upendo ilianzishwa Kwa nguvu za wananchi mwaka 2007 yenye jumla ya madarasa Saba ,ikiwa na idadi ya wanafunzi 352 ikiwa na wanafunzi wavulana 158 na wasichana 194 huku kukiwa na jumla ya walimu watano ikiwa wakike 2 na wakiume 3 .
Shule ya msingi Upendo IPO katika Kijiji Cha Mputa kata ya Mputa na kitendo Cha mbunge Kutoa madawati yenye thamani ya shilingi 1,650,000 na mifuko ya smenti yenye thamani ya shilingi 700,000 katika shule hiyo imesaidia kupunguza changamoto zilizopo katika shule hiyo.
Mwisho.
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: 2 Barabara ya Boma, S.L.P 55, 57382 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0767519181
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.