MKuu wa wilaya Namtumbo mkoani Ruvuma amepanga kuanzisha operesheni panda mihogo kwa ajili ya kukabiliana na upungufu wa chakula ambao unaweza kujitokeza hapo baadae
Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Dkt.Julius Kenneth Ningu ameserma mpango huo utawasilishwa katika vikao vya kisheria vya halmashauri ili wazo hilo la kuhamasisha kilimo cha zao la mihogo liweze kupata Baraka za vikao husika
Kassimu Gunda diwani wa kata ya Likuyu alidai wazo hilo la mkuu wa wilaya ni wazo zuri na kuhaidi kumpa ushirikiano katika vikao vya kisheria vya Halmashauri hiyo ili wazo hilo liweze kupitishwa na kuungwa mkono na madiwani wa Halmashauri hiyo
Gunda alidai wazo hilo litasaidia wananchi wa wilaya ya Namtumbo kiuchumi ,pamoja na kukabiliana na upungufu wa chakula kwa musimu ambao hali ya hewa itakuwa sio wezeshi kwa mazao endapo kama kutatokea ukame .
Mpango wa kuanzisha operesheni ya kilimo cha mihogo katika Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo inategemea kuanzishwa katika msimu huu wa 2022/2023 ili kuifanya wilaya ya Namtumbo kujikinga na upungufu wa chakula ambao unaweza kutokea endapo kama kutatokea na ukame.
Aidha mpango kwa mujibu wa mkuu wa wilaya huyo alidai kuwa utakuwa shirikishi kwa kuwashirikisha viongozi ngazi ya wilaya,kata na vijiji ili kuweza kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kulima mashamba ya mihogo.
Salumu Kiyomoyomo wa kijiji cha Kitanda pamoja na kumpongeza mkuu wa wilaya huyo alisema wazo hilo la mkuu wa wilaya ni wazo la kuifanya wilaya kujiimarisha kiuchumi pamoja na kujikinga na uhaba wa chakula .
Kiyomoyomo alimwomba mkuu wa wilaya huyo kuishauri Halmashauri kuweza kupata mbegu ya muda mrefu inayoweza kukaa kwa muda mrefu ardhini bila kuharibika tofauti na mbegu za mihogo ya sasa iitwayo kiroba ambayo haiwezi kukaa kwa muda mrefu.
Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo ina jumla ya kata 21 ambapo kata hizo wananchi wake wakihamasishwa kulima zao la muhugo itaifanya wilaya kuwa na chakula cha kutosha na kuwa na ziada kubwa ya chakula.
Mwisho.
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: 2 Barabara ya Boma, S.L.P 55, 57382 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0767519181
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.