Akitoa taarifa ya mradi wa hewa ukaa katika mafunzo ya kuwajengea uwezo na uelewa waheshimiwa madiwani ,wadau wa maendeleo na wakuu wa idara na vitengo wa halmashauri ya wilaya ya Namtumbo afisa wanyama pori na misitu wa halmashauri ya wilaya hiyo Prisca Msuha alisema mradi wa hewa ukaa utaifanya Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo kumwagiwa mabilioni ya fedha wakati mradi utakapoanza kazi.
Priska katika taarifa yake alidai mradi wa hewa ukaa utatekelezwa katika vijiji vinavyopatikana katika jumuiya za uhifadhi za wanyamapori za kimbanda,kisungule na Mbarangāandu zilizopo katika kata za Kitanda,Mgombasi,Ligera,Msisima,Mchomoro,Magazini,Lusewa na Likuyuseka.
Priska alisisitiza idara yake kwa kushirikiana na wadau wa uhifadhi TAWA,TANAPA,na TFS walishatoa mafunzo kwa viongozi wa vijiji, watendaji wa vijiji ,kata na wadau mbalimbali wa maendeleo katika ngazi ya kata na vijiji kuhusu mpango wa hewa ukaa .
Aidha Priska alifafanua lengo la mpango wa hewa ukaa ni kuzinufaisha jamii inayotunza misitu ambayo hewa yake kutoka katika misitu hiyo ndiyo inayosaidia kunyonya hewa chafu inayozalishwa katika viwanda vikubwa duniani ili waendelee kulinda na kupanda miti katika mazingira yao .
Diwani wa kata ya Likuyuseka Kassim Gunda alisisitiza kuwepo kwa uwazi katika kutekeleza mpango huo na kuagiza idara inayohusika kushirikisha jamii moja kwa moja ili kuepuka sintofahamu ambayo inaweza kutokea kama jamii ambayo ndiyo yenye maeneo ya uhifadhi kutofahamu vizuri juu ya mpango huo.
Diwani huyo alidai ushirikishwaji wa jamii katika kutekeleza mpango huo upewe kipaumbele kwani jamii ndio inayotakiwa kupatiwa elimu zaidi kutokana na maeneo ya uhifadhi hayo yapo katika vijiji ambapo jamii hiyo ndiyo ipo ili kuepusha migogoro ambayo inaweza kujitokeza hapo baadae alisema diwani huyo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Jumma Pandu aliwasisitizia waheshimiwa madiwani kwenda kuelimisha jamii katika maeneo yanayoenda kutekeleza mradi huo kuelimisha jamii umuhimu wa mradi huo kwa jamii,halmashauri na serikali kwa ujumla.
Pandu aliwataka madiwani kwenda kuwaelekeza wananchi matumizi ya maeneo na kuzingatia kutochanganya matumizi ya maeneo na kwenda kuwasisitizia wananchi kutumia maeneo kama yalivyopangwa katika mpango wa matumizi bora ya ardhi yao.
Nchini Tanzania mradi wa hewa ukaa unatekelezwa katika wilaya za Kiteto,Tanganyika ,karatu na Makame ambapo kwa wilaya ya Tanganyika yenye lenye eneo la msitu wa kilomita 2500 hunufaika na shilingi 3,000,000,000 kwa mwaka.
Mwisho.
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: 2 Barabara ya Boma, S.L.P 55, 57382 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0767519181
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
HakimilikiĀ©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.