NAMTUMBO WAPOKEA VITAMBULISHO 60,857 VYA TAIFA
Akizungumza katika ofisi ya NIDA katika Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma ,Afisa msajiri wa vitambulisho vya Taifa wilaya Thobias Nangalaba alisema ofisi yake imepokea vitambulisho ....60,857..........Kwa ajili ya wananchi wa wilaya ya Namtumbo.
Tobias Nangalaba alisema vitambulisho hivyo vinapokelewa Kwa awamu ,huku akiwahimiza wananchi kujiandikisha ili waweze kujipatia vitambulisho vya Taifa.
Nangalaba alidai wananchi wanaweza kujitokeza kujiandikisha wakati watumishi wa ofisi yake wanapowafuata wananchi vijijini au Kuja ofisi ya NIDA Moja Kwa Moja iliyepo Katika Jengo la Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo
Sefu Luambano kijana kutoka katika Kijiji Cha Kitanda wilaya Namtumbo alikutwa katika ofisi za NIDA Kuja kujiandikisha alisema kukosa kitambulisho Cha Taifa ni kujikwamisha katika fursa mbalimbali ,Kwa kuwa kitambulisho hicho ni muhimu Kwa mambo mengi Kwa sasa.
Sharifu Ally Mfaume kijana kutoka katika mamlaka ya mji mdogo wa Namtumbo alisema amelazimika kujiandikisha ili kupata kitambulisho Cha Taifa au Namba ya kitambulisho ili iweze kumwezesha kupata cheti Cha kuzaliwa ..
Ugawaji wa vitambulisho vya Taifa(NIDA) vinagawiwa Kwa wananchi katika kata 21 za wilaya ya Namtumbo kupitia ofisi za watendaji wa vijiji.
Ofisi ya usajiri wa vitambulisho vya Taifa wilaya ya Namtumbo Ina wataka wananchi wote wenye vitambulisho viliyofika katika ofisi za watendaji wa vijiji kujitokeza Kwa wingi kuchukua vitambulisho vyao .
Mwisho.
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: 2 Barabara ya Boma, S.L.P 55, 57382 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0767519181
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.