NG”OMBE 324 NA PUNDA WA 5 WAKAMATWA NAMTUMBO
Ng’ombe 324 na Punda wa 5 wamekamatwa katika kijiji cha kitanda wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma kwa kuingia mkoa wa Ruvuma kinyemera bila vibali vilivyowaruhusu kuingiza mifugo yao katika mkoa wa Ruvuma wakitokea mkoani Morogoro wilaya ya Malinyi.
Afisa mifugo wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Paul Ambokile alikiri kukamatwa kwa mifugo hiyo katika kijiji cha kitanda na kudai kuwa wafugaji hawakufuata utaratibu wa uingizaji wa mifugo kutoka mkoa mwingine na kuingiza mkoa mwingine.
Hata hivyo Ambokile alidai waingizaji wa mifugo hiyo walilipa faini ya kuingiza mifugo bila vibali na zoezi la kuwarudisha wafugaji pamoja na mifugo yao lilisimamiwa na uongozi ngazi ya Mkoa wa Ruvuma kwa kuwasiliana na uongozi wa ngazi ya mkoa wa Morogoro .
Afisa mtendaji wa kijiji cha kitanda Ayubu Muhuwa alisema Ng’ombe na punda hao walikuwa katika maeneo ya msitu wa hifadhi ya kijiji cha kitanda Mtaungana eneo ambalo limetengwa na kijiji cha kitanda kwa ajili ya matumizi bora ya ardhi.
Mhuwa alidai taarifa za wafugaji kuchunga mifugo yao katika maeneo ya hifadhi zilitolewa katika mamlaka husika ambapo wajumbe wa serikali ya kijiji kwa kushirikiana na kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma waliwakamata wafugaji hao waliokuwa na Ng’ombe 324 na Punda wa 5 katika hifadhi ya kijiji Mtaungana.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma ACP. Marco Chillya walikiri kukamata mifugo329 na wafugaji waliotokea wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro na kuingia kijiji cha kitanda wilaya ya Namtumbo bila kuwa na vibali vilivyowaruhusu kuingiza mifugo katika mkoa wa Ruvuma na hivyo pamoja na kuwataka kulipa faini waliwasimamia wafugaji hao kurudisha mifugo yao wilaya ya Malinyi Mkoa wa Morogoro.
kijiji cha kitanda ni kijiji cha wilaya ya Namtumbo mkoa wa Ruvuma kilichopakana na wilaya ya Malinyi mkoa wa Morogoro ambapo wafugaji hutumia kupitisha mifugo yao kutoka wilaya ya Malinyi na kuingiza mkoa wa Ruvuma kupitia kijiji hicho.
Mwisho
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: S.L.P 55 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0765142640
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.