NYARAKA ZA MANUNUZI UJENZI WA BARABARA NAMTUMBO MJINI ZAMRIDHISHA KIONGOZI MBIO ZA MWENGE
Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Godfrey Eliakimu Mnzava aliridhishwa na nyaraka za Manunuzi yaliyofanywa na Tarula Wilaya ya Namtumbo wakati wa kutekeleza mradi wa ujenzi wa Barabara ya Lami Namtumbo Mjini.
Mnzava alidai kuridhishwa na Tarura Wilaya ya Namtumbo kwanza Kwa kufuata taratibu,kanuni na sheria za zabuni katika kuwapata wazabuni lakini pia kutumia mfumo wa Manunuzi ya umma katika Kila Hatua.
Pamoja na hayo Mnzava alikagua barabara ya Lami yenye urefu wa kilomita 1.6 iliyojengwa Kwa zaidi ya milioni 889 na kuridhika kuweka jiwe la msingi katika barabara hiyo.
Mhandisi Fabian Lugalaba Meneja wa Tarura Wilaya ya Namtumbo alisema madhumuni ya kujenga barabara ya Lami kilomita 1.6 ni kuimarisha mawasiliano kati ya kitongoji Cha Namabengo na Bomani na hasa kuboresha mandhari ya mji wa Namtumbo Kwa ujumla.
Lugalaba alidai ujenzi wa Barabara ya Lami Namtumbo Mjini ulihusisha ujenzi wa matabaka ya changarawe, Lami nyepesina kokoto Pamoja na uwekaji wa taa 43 za Sola barabarani.
Ujenzi mwingine ulihusisha ujenzi wa karavati mita 101,uwekaji wa alama za barabarani 10 na ujenzi wa mifereji ya barabara mita za mraba 3084 alisema Lugalaba.
Ally Lyuma mkazi wa mji wa Namtumbo Pamoja na kumpongea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa kutoa fedha alisema ujenzi huo wa Barabara ya Lami kilomita 1.6 umebadilisha mandhari ya mji wa Namtumbo na kuanza kuvutia.
Lyuma aliwapongeza TARURA Wilaya ya Namtumbo Kwa kusimamia vyema ujenzi wa Barabara hiyo na kuwaomba kutenga fedha katika bajeti ili kuendelea kujenga barabara za Lami katika mji wa Namtumbo.
Kauli Mbiu ya mwenge wa uhuru mwaka huu 2024 ni 'Kutunza Mazingira na kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa Kwa ujenzi wa Taifa endelevu.
Mwenge wa uhuru Wilayani Namtumbo umemaliza mbio zake Kwa kutembelea miradi,kukagua,kuzindua na kuweka mawe ya msingi umbali wa kilomita 170 na kukabidhi Halmashauri ya Songea katika Kijiji Cha Lipaya.
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: 2 Barabara ya Boma, S.L.P 55, 57382 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0767519181
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.