Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan amewafariji watoto wenye Mahitaji Maalum kutoka katika Shule ya msingi Namtumbo iliyopo Wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma kwa kuwapatia Mahitaji muhimu hasa katika msimu huu wa sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya.
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mhe. Ngollo Malenya amekabidhi Zawadi hizo Disemba 27, 2024 wakati alipo kwenda kuwatembelea watoto hao katika Maeneo ya Shule ya Msingi Namtumbo ambapo Katibu tawala wa Wilaya ya Namtumbo Ndg. Francis Mgoloka amekabidhi zawadi hizo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya.
"Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ni kawaida yake inapofika msimu wa Sikukuu kama hizi kutoa zawadi Kwa watoto, wazee na wananchi ili waweze kufurahia sikukuu kwa pamoja, na leo ameona ni vema kuwafikia watu wa Namtumbo" amesema Mgoloka
Aidha Katibu tawala Wilaya ya Namtumbo Ndg. Francis Mgoloka amewataka wananchi kufurahia sikukuu za mwisho wa mwaka kwa kuwajali watu wenye mahitaji Maalum ikiwa pamoja na kuwapa msaada na mahitaji mbalimbali.
Hata hivyo Dyness Magoyo Mkuu wa Shule ya Msingi Namtumbo ametoa Shukrani zake za Dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mhe. Dkt. Samia Suhuhu Hassan kwa kuwajali na Kuwakumbuka Watoto wenye Mahitaji maalum kutoka katika Wilaya ya Namtumbo uku akitoa wito kwa wananchi na mashirika mbalimbali kuendelea kuwakumbuka na kuwajali kwani kazi hii sio ya Serikali pekee lazima wananchi waungane kuwasaidia watoto wenye mahitaji maalum na watoto Yatima.
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: 2 Barabara ya Boma, S.L.P 55, 57382 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0767519181
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.