RC RUVUMA AWATAKA WAKUU WA WILAYA KUJIPANGA KIMKAKATI MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2024.
Akiongea kwenye kikao Cha awali na wadau mbalimbali katika ukumbi wa Manispaa ya Songea Kanali Ahmed Abbas Ahmed aliwataka wakuu wa Wilaya kujipanga kimkakati kuukimbiza mwenge wa uhuru katika Mkoa wa Ruvuma.
Kanali Ahmed Abbas Ahmed alisema Mwenge wa uhuru ni itifaki ya Mheshimiwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivyo aliwaagiza wakuu wa Wilaya kujipanga kimkakati ili uwepo wa mheshimiwa Raisi katika Mkoa wetu upewe uzito wa hali ya juu.
Hata hivyo Kanali Abbas alihimiza kuwepo kwa mikakati ya ushindi itakayoifanya mkoa wa Ruvuma kushinda Kwa kishindo katika mbio za mwaka huu 2024 alisema Kanali Abbas.
Awali Mratibu wa mbio za mwenge wa uhuru Mkoa wa Ruvuma Zuberi Mshamu alisema ukimbizaji wa mwenge wa uhuru unakuwa na sura ya mashindano ambapo mikoa imegawanywa katika Kanda 5 na Mkoa wa Ruvuma upo katika Kanda ya 3 inayojumuisha mikoa Sita ambayo ni Ruvuma ,Singida,Dodoma,Manyara,Kagera na Mara.
Katika mashindano ya mbio za mwenge wa uhuru Kwa mwaka 2023 Mshamu alisema Mkoa wa Ruvuma ulishika nafasi ya 10 (kumi)kitaifa Kwa kupata wastani wa alama76.27.
Katika kikao hicho waratibu wa mwenge wa uhuru katika Halmashauri 8 za mkoa wa Ruvuma ziliwasilisha taarifa ya Maandalizi ya mapokezi ya mwenge wa uhuru , Kwa kuweka wazi miradi itakayotembelewa na mwenge wa uhuru Kwa mwaka 2024
Mkoa wa Ruvuma utapokea mwenge wa uhuru tarehe 8 mwezi Juni 2024 katika Kijiji Cha Sauti Moja kilichopo Wilaya ya Tunduru kutoka Mkoa wa Mtwara na kuukabidhi mkoa wa Njombe tarehe 16 mwezi Juni 2024 Kijiji Cha Mavanga Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa.
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: 2 Barabara ya Boma, S.L.P 55, 57382 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0767519181
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.