Siku tano za Matembezi ya hiari Namtumbo
Chama Cha Mapinduzi wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma kinafanya matembezi ya hiari ya siku tano yakianzia uwanja wa majimaji Manispaa ya Songea na kumalizikia katika ofisi ya Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Namtumbo .
Lengo la matembezi hayo ni kuunga mkono juhudi za Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dkt Samia Suluhu Hassan na kumuenzi baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere .
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Namtumbo Zuberi Lihuwi alisema vijana wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Namtumbo wameamua kufanya matembezi ya hiari wakiwa na lengo la kuunga mkono juhudi za Raisi wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na kumuenzi mwalimu Julius Kambarage Nyerere .
Lihuwi alidai matembezi hayo yatakuwa ya siku tano kuanzia tarehe 16 mwezi huu 2023 mpaka tarehe 20 mwezi huu wa kumi 2023 ambayo yatachukua muda wa siku tano.
Aidha Kwa Mujibu wa Ratiba ya matembezi hayo siku ya kwanza ya tarehe 16 mwezi huu yalianzia uwanja wa majimaji na kuishia katika Kijiji Cha Mtakanini wilayani Namtumbo.
Tarehe 17 mwezi huu ikiwa ni siku ya pili ya matembezi hayo yataendelea na safari kupitia katika vijiji vya wilaya ya Namtumbo na kuishia katika shule ya Sekondari Namabengo.
Hata hivyo matembezi hayo Kwa siku ya Tatu yatatoka Namabengo siku ya tarehe 18 na kwenda kuhitimisha ziara yake katika shule ya msingi Luegu na tarehe 19 matembezi hayo yataishia shule ya Sekondari Kawawa iliyopo katika Kijiji Cha Suruti kata ya Namtumbo .
Matembezi ya hiari ya umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi wilayani Namtumbo yatahitimishwa tarehe 20 mwezi huu katika ofisi za Chama hicho wilayani Namtumbo baada ya matembezi hayo kutoka katika shule ya Sekondari Kawawa iliyopo wilayani humo..
Mwisho.
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: 2 Barabara ya Boma, S.L.P 55, 57382 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0767519181
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.