TAIFA LISILOJUA HISTORIA YAKE NI SAWA NA TAIFA LILILOKUFA
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea Kapenjama Ndile wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya kuwakumbuka mashujaa 67 walionyongwa na Wajerumani wakati wa Vita vya Majimaji Manispaa ya Songea.
Kapenjama alisema Taifa Lisilokuwa na historia yake ni sawa na Taifa lililokufa huku akiwataka wananchi Kujua historia ya Mashujaa wa Majimaji waliopinga unyanyasaji kutoka kwenye utawala wa Kijerumani na kupigana vita na kupelekea kunyongwa kwao.
Noel Lwoga Mkurugenzi wa Makumbusho Taifa alidai tafsiri ya kuwaenzi na kuwakumbuka mashujaa ilitolewa na Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipo agiza kujengwa Kwa Minara kuwakumbuka babu zetu waliopigania uhuru katika Nchi hii mjini Mwanza mwaka 1980
Mwalimu Nyerere akiwa Mwanza tarehe 6 mwezi Juni 1980 alipitisha adhimio la kujenga Kwa Minara kuwaenzi na kuwakumbuka babu zetu waliopigania uhuru wa nchi hii na kupelekea kuwauwa Kwa kupigwa risasi au kunyongwa kwao.
Chifu Zulu Gama(1)Pamoja na kuwakaribisha Machifu wenzake kutoka Nchini Malawi alisema Kwa mujibu wa taratibu za Mila na desturi za Kingoni kuwakumbuka marehemu ni sehemu ya kuomba matatizo mbalimbali yaweze kutatuliwa katika familia au ukoo.
Benedicto Wakulyamba Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Pamoja na mambo mengine alisema Wizara hiyo kupitia kumbukizi hizo hutumika pia kuibua shughuli za Utalii na kutangaza shughuli za Utalii katika nchi yetu.
Awali akisoma taarifa ya baraza la Makumbusho ,Katibu wa baraza hilo Abbas Mpumule Chitete alisema baraza hilo limejikita katika kuwakumbuka mababu waliopigania uhuru ,Kujikita katika kuhifadhi Mila na desturi Pamoja na uhifadhi wa Mali kale.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas alimwakilisha Waziri wa Maliasili na Utalii katika Maadhimisho hayo Pamoja na kumpongea Rais alifafanua dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hasan kuanzisha Mazungumzo na Serikali ya Ujerumani ili kurudishiwa Mali kale zilizochukuliwa Nchini ili Watanzania waweze kunufaika na mali kale zao kupitia Utalii wa ndani badala ya Mali kale hizo kuhifadhiwa huko Ujerumani.
Kumbukizi ya kuwaenzi Mashujaa walionyongwa katika vita vya Majimaji Manispaa ya Songea hufanyika Kila mwaka mwezi februali ambapo huambatana na tamasha la kutangaza Utalii, tamasha la kuenzi Mila na desturi na kilele chale ni tarehe 27 mwezi februali Kila mwaka .
Kauli mbiu ya madhimisho hayo ni "Makumbusho ya Majimaji na ukombozi wa bara la Afrika na matumizi ya Rasilimali zake,urithi wetu Kwa maendeleo ya Utalii na Uchumi"
Mwisho
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: 2 Barabara ya Boma, S.L.P 55, 57382 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0767519181
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.