VIONGOZI WAMWAGA SIFA USIMAMIZI UJENZI DKT .SAMIA.
VIONGOZI ngazi ya kitaifa ,Mkoa na wilaya wasifu usimamizi wa ujenzi wa Sekondari ya Dkt. Samia Suluhu Hassan Kuwa ni sekondari iliyojengwa Kwa kiwango Cha Hali ya juu inayolingana na fedha iliyotolewa.
Ziara ya Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa katika shule hiyo alifurahishwa na ujenzi huo lakini ziara ya mwenyekiti wa UWT taifa Mary Chatanda naye alisifu usimamizi wa ujenzi huo pamoja na kamati ya siasa Mkoa wa Ruvuma ikiongozwa na Komred Oddo Mwisho mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Ruvuma naye alisifu usimamizi makini katika ujenzi wa sekondari hiyo.
Sekondari ya Dkt Samia Suluhu Hassan ilifunguliwa mwezi Agosti mwaka huu Kwa wanafunzi wanaosoma tahasusi ya Sanaa pamoja na tahasusi ya Sayansi.
Afisa elimu sekondari Michael Lyambilo alisema Shule hiyo Kwa mara ya kwanza imefunguliwa na kupangiwa na Serikali kupokea wanafunzi 249 na walioripoti na kuendelea na masomo ni wanafunzi 200. Hata Hiv
Hata hivyo Lyambilo alidai shule hiyo inamiundombinu mizuri kiasi ambacho kinarahishia wanafunzi wa shule hiyo kuwa na mazingira mazuri ya kupata elimu alisema Lyambilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Chiriku Hamis Chilumba pamoja na kuipongeza Serikali ya awamu ya Sita ya Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa kuleta fedha nyingi katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikiwemo na ujenzi wa sekondari ya wasichana Mkoa wa Ruvuma iliyopewa jina la Dkt Samia Suluhu Hassan iliyojengwa wilaya ya Namtumbo.
Chilumba Pamoja na mambo mengine alisema Serikali inaleta fedha nyingi katika miradi wilayani humo akitaja mradi wa ujenzi wa sekondari ya Dkt Samia awali walipokea shilingi bilioni 3 na Sasa zimepokelewa Tena bilioni 1.1 Kwa ajili ya kuendelea miundombinu shuleni hapo.
Aidha Chilumba alidai Serikali Kwa Sasa inatoa fedha nyingi na kazi iliyopo katika ofisi yake ni kuhakikisha wanaisimamia miradi yote inayopewa fedha itekelezwe Kwa kiwango kinachostahili na sio vinginevyo alisema Chilumba.
Usimamizi wa miundombinu katika ujenzi wa shule hiyo ya Sekondari unafurahishwa na viongozi wa kitaifa,Mkoa na wilaya kutokana na ubora uliopo wa majengo hayo ukilinganisha na fedha zilizotolewa.
Mwisho.
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: 2 Barabara ya Boma, S.L.P 55, 57382 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0767519181
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.