Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya NamtumboNdg. Philemon Mwita Magesa amesema kuwa kilichotokea katika kuhusiana na Kuenguliwa kwa baadhi ya Wagombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) SIO za kweli na inabidi kupuuzwa.
Akizungumza na waandishi wa Habari Mapema leo tarehe 12 Novemba 2024 katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo, Magesa amesema "Wagombea wa CHADEMA baadhi hasa ambao wametokea kata ya Likuyuseka wameonekana wakisema kwamba fomu zao Hazijabandikwa
Nipende kuchukua fursa hii ndugu waandishi wa Habari kuwaambia kwamba wagombea hao wa CHADEMA kweli walijitokeza kuchukua Fomu, wapo wagombea kumi na tatu (13) Mgombea wa mwenyekiti wa kijiji mmoja (1) wagombea wanane (8) wa kitongoji na Wapo wagombea Wanne (4) katika wajumbe mchanganyiko jumla wanakuwa Kumi na tatu (13), Sasa wanaposema kwamba fomu zao zote hazikubandikwa
Nini kilitokea? Wagombea wote hao kumi na tatu (13) kwa mujibu wa kanuni za Uchaguzi, Unapochukua fomu ya kugombea na ukadhaminiwa na chama chako ni lazima fomu hiyo uirejeshe kwa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi ambaye ni Mtendaji wa kijiji husika.
Wagombea hao CHADEMA ndugu Waandishi wa Habari HAWAKUREJESHA FOMU wote Kumi na tatu"
Hata hivyo Magesa amewaomba Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo kushiriki kikamilifu katika zoezi la Uchaguzi ifikapo tarehe 27 Novemba 2024 ili waweze kuchagua viongozi wanao wahitaji.
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Anuani: 2 Barabara ya Boma, S.L.P 55, 57382 NAMTUMBO
Simu ya Mezani: 0252675008
Simu ya Mkononi: 0767519181
Barua Pepe: ded@namtumbodc.go.tz
Hakimiliki©2021Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Haki zote Zimehifadhiwa.