WANAFUNZI WA SHULE YA WASICHANA YA MUFINDI WATEMBELEA BANDA LA NAMTUMBO NANENANE - MBEYA
Tarehe ya Kuweka: August 7th, 2024
Wanafunzi kutoka katika shule ya Wasichana ya Mufindi iliyopo Mkoani Iringa wametembelea katika Banda la Seedco Kutoka Wilayani Namtumbo Kwaajili ya Kujifunza Masuala mbalimbali kuhusu kilimo cha kisasa.
Wanafunzi hao wamekutana na Mtaalamu wa Mbegu za Kilimo Bw. Sekwese ambapo alikuwa akijibu Maswali mbalimbali ambayo yalikuwa yakiulizwa na Baadhi ya Wanafunzi hao katika viwanja vya John Mwakangale Jiji Mbeya.